KUZA NYWELE KWA MAJI YA MCHELE


Inashangaza ndio, na ina weza isiaminike lakini huo ndio ukweli. Maji ya mchele yana faida kubwa katika nywele unaweza kuuliza kivipi na nani yamemsaidia, inasemekana kabila la Yao kutoka kijiji cha Huangluo Nchini China ndilo kabila ambalo lina wanawake wenye nywele ndefu zaidi duniani, ambapo wanaweza kufunga nywele zao kama kiremba

Wanawake hawa wanaamini kutumia maji ya mchele kuoshea nywele zao ndiko kunako fanya nywele zao kuwa ndefu zenye afya na kutokupatwa kwa mvi mpaka katika miaka ya 80. Huko nchini china una weza kununua maji ya mchele na pia kuna site mbali mbali duniani wanayauza kwa $23 sawa na Tsh2,6933 lakini pia unaweza kuandaa mwenyewe.


Unacho takiwa kufanya ni wakati una pika mchele wako (wali) ongeza maji kidogo tofauti na yale uliyo yazoea kisha yakisha chemka na kuanza kuwa mazito na kubadilika rangi kuwa ya mchele punguza kwenye kibakuli na uyaache ya poe, baada ya hapo yakisha poa paka kwenye nywele zako na ukae nayo kwa muda wa dakika 3-5 na uoshe kwa maji masafi.

Maji ya mchele husaidia kukuza, kulinda nywele zisikatike na zilizokatika kurudi katika hali yake ya kawaida pamoja na ku ng’arisha nywele.

0/Post a Comment/Comments